Posts

MAGEUZI YA ELIMU TANZANIA YAVUTIA NCHI NYINGINE KUJIFUNZA

Image
Mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu nchini, hususan mafunzo ya Amali yameanza kuvutia mataifa mengine barani Afrika kuja kujifunza namna yalivyofanyika na utekelezaji wake. Hayo yalibainishwa jijini Dodoma kufuatia ziara ya Waziri wa Elimu ya Juu, Utafiti, Sayansi na Teknolojia kutoka Jamhuri ya Gambia, Prof. Pierre Gomez ambaye alisema kuwa lengo la kufika Tanzania ni kujifunza mbinu zilizotumika katika kufanya maboresho na maugezi makubwa katika sekta ya elimu. Waziri huyo alisema kuwa Benki ya Dunia iliishauri nchi hiyo kuja Tanzania ili kujionea namna utekelezaji wa Sera, mikakati na miradi mbalimbali katika sekta ya elimu ili kuwawezesha kutekeleza miradi yao kwa ufanisi na tija. “Tumeshuhudia ujenzi wa miundombinu na mifumo ya mafunzo ya vitendo yenye tija katika vyuo mbalimbali ikiwemo DIT, VETA na Taasisi, tunaamini kunufaika zaidi kupitia ushikiano katika nyanja mbalimbali za mafunzo” alisema Prof. Gomez. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzan...

DKT. BITEKO ASEMA TANZANIA INA USALAMA WA CHAKULA, AWAPONGEZA WAKULIMA

Image
* Asema Serikali inatambua Vyama vya Ushirika ni muhimu kuunganisha nguvu za wananchi na kujiendeleza kiuchumi * Mauzo ya nje ya kahawa na tumbaku 2023/2024 yaongezeka hadi Dola za Marekani 19,300,000 * Maono ya Rais Samia yaanza kuonekana sekta ya kilimo yachangia GDP asilimia 26 * Aziagiza Wizara za Fedha na Kilimo kupata ufumbuzi wa bei za mazao   Na. Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewapongeza wakulima nchini kwa jitihada zao za kuzalisha mazao kwa wingi na hivyo kusaidia nchi kuwa na usalama wa chakula ikiwa ni pamoja na kuwezesha sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.  Dkt. Biteko alitoa pongezi hizo jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani. “Leo sekta ya kilimo ina mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu, tunazungumza mchango wa GDP wa asilimia 26, tunazungumza mazao ambayo yanatupa usalama wa ch...

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA UPADIRISHO JIMBO KATOLIKI DODOMA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki kushiriki katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma.  Misa hiyo Takatifu imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya.  Askofu Kinyaiya aliwasisitiza waumini kujitokeza katika kupiga kura kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu watakaowatumikia kwa miaka mitano ijayo. Pia ametoa rai ya matumizi sahihi ya akili mnemba (AI) ili kuepusha maovu na udanganyifu katika jamii. Jumla ya Mashemasi watatu wamepata daraja la Upadre katika Misa hiyo ambao ni Padre Joseph Ibrahim, Padre Sajilo Mark pamoja Padre Damian Mtanduzi. Aidha, Misa hiyo imeambatana na uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa jengo la ...

TANESCO SACCOS YAIGUSA SEKTA YA AFYA KWA KUTOA MASHUKA YENYE THAMANI YA MILIONI 23 JIJINI DODOMA

Image
Na. Janeth Raphael, MichuziTv -Dodoma  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema pamoja serikali kufanya kazi kubwa hasa katika Sekta ya Afya ikiwemo ununuzi wa vifaa, Dawa, Majengo na miundombinu na watumishi lakini bado safari ya maendeleo katika sekta hiyo huwa haiishi kutokana na watu kuongezeka na magonjwa kubadilika. RC Senyamule alisema hayo jijini Dodoma katika hafla fupi ya kupokea Mashuka 300 ya kuhudumia wagonjwa waliopo katika hospitali za Mkoa wa Dodoma yaliyotolewa na wana Ushirika wa Tanesco Saccos.  Alisema kuwa kutoka na uhitaji wa kila siku serikali hata kama ingenunua mashuka mengi kiasi gani bado yasingeweza kudumu siku zote kwasababu ingefika muda yangechakaa na kuhitajika mengine. “Tunajua kuwa serikali yetu chini ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia imefanya kazi kubwa sana katika Sekta ya Afya. Zipo sekta nyingine lakini katika sekta ya Afya imefanya makubwa kuanzia Vifaa,Majengo,Miundombinu,Watumishi na vitu vingine vingi, lakini tunafahamu ...

MAWAKILI NCHINI WATAKIWA KWENDA KUZISOMA SHERIA ZA UCHAGUZI MKUU

Image
Na. Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma Mawakili nchini Tanzania wametakiwa kwenda kuzisoma sheria za Uchaguzi Mkuu, ili waweze kuwasaidia kujaza fomu wagombea waliojitokeza kutia nia, lakini pia kutatua migogoro itakayowasilishwa kwa kukosa uelewa katika Mahakama mbalimbali hapa nchini. Jaji Mkuu wa Tanzania ,George Masaju aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akiwathibitisha na kuwapokea Mawakili 449 wakiwemo wa Serikali na wa kujitegemea, ikiwemo kuorodheshwa rasmi katika orodha ya mawakili waliothibitishwa hapa nchini. Aidha, aliwataka Mawakili hao kwenda kufanya kazi katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam na Dodoma ambayo ina mawakili wa kutosha, ili kuepuka kuitwa vishoka hasa ukizingatia soko la Kada hiyo ni kubwa kwa sasa. Alisema kuwa kuna sheria nyingi zikiwemo za Polisi, Uchaguzi na nyingine. Na kusema kuwa Mawakili wanapaswa kutumia muda mwingi kuzisoma na kuzielewa ili waweze kutumia fursa ya kuwasaidia wagombea mbalimbali waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea na...

RAIS SAMIA ANAPENDA KUFANYA KAZI NA VIONGOZI WA DINI - DKT. BITEKO

Image
  📌 Asisitiza milango ya Rais Samia ipo wazi kwa ajili ya mazungumzo kwa mustakabali wa Taifa 📌 Asema Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Taasisi za dini 📌 Serikali kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini kuchochea maendeleo 📌 Uchaguzi ni daraja la amani na maendeleo si chanzo cha mifarakano – Baba Askofu Shoo 📌 CCT yahimiza maadili ya kisiasa, utulivu wa jamii na kampeni za kistaarabu 📌 Taasisi za dini Afrika zatajwa kuchangia maendeleo ya sekta ya afya kwa 30%- 70% Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile. Dkt. Biteko aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akimwakilisha  Rais, Dkt. Samia Su...

Halmashauri ya Jiji la Dodoma yashiriki maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma inashiriki maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayojumuisha Taasisi za Serikali, Bunge na Mahakama, katika uwanja wa Chinangali Park jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yanalenga kuonesha uwajibikaji wa taasisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kutoa elimu mbalimbali. Hayo yalisemwa na Afisa Utumishi, Patrick Bashemela alipokuwa akitoa utambulisho wa huduma zinazopatikana katika banda la halmashauri. “Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanatupa fursa nzuri ya kuonesha namna huduma zetu zinawafikia wananchi, banda letu linatoa huduma ya ukataji wa leseni ya biashara, elimu ya matumizi ya mfumo wa Tausi, elimu ya juu ya mikopo ya asilimia 10 na huduma ya uuzaji viwanja. Huduma zote muhimu zinazotolewa halmashauri, zitapatikana hapa kwa siku zote za maadhimisho” alisema Bashemela. Alimalizia kwa kuwakaribisha watumishi wote na wananchi kutembelea banda la halmashauri ili kupata elimu ya huduma mba...

Mexime awaonya mastaa Dodoma Jiji FC, aitaja nafasi ya tano

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA. Kocha Mkuu wa Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, Mecky Mexime amewataka wachezaji wa timu hiyo kuzingatia yale waliyojifunza kwenye uwanja wa mazoezi ili kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Singida Black Stars na waweze kutimiza malengo waliyojiwekea kwa msimu huu. Mexime aliyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo ambapo walima zabibu wa Dodoma Jiji FC watavaana na kikosi cha Singida Black Stars ikiwa ni duru ya lala salama ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, mchezo unaotarajiwa kuvurumishwa majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. “Tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huu ili tuweze kusogea nafasi za juu zaidi kwasababu nafasi ya tano bado iko wazi kwa yeyote atakayechanga karata zake vizuri ataweza kuishika. Sisi Dodoma Jiji FC mipango yetu ni kufika nafasi ya tano, kikubwa ni wachezaji kuzingatia kile tulichojifunza kwenye uwanja wa mazoezi na kuja kukionesha uwanjani” alisema Mexi...

Jiji la Dodoma lafikisha 93% ya ukusanyaji Mapato

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufikia asilimia 93 ya makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2025 na kusema kuwa ukusanyaji huo unatoa matumaini ya kufikia lengo ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha. Pongezi hizo alizitoa katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Senyamule alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya uchambuzi wa mapato ya mamlaka za serikali za mitaa kwa Mkoa wa Dodoma uliofanywa na wataalam wa ofisi yake hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2025 Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilikuwa imekusanya asilimia 93. “Hivyo, niendelee kusisitiza menejimenti ya halmashauri kuongeza nguvu ya ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha kuwa asilimia saba iliyobaki inakusanywa kabla ya tarehe 30 Juni, 2025. Wataalamu wangu ...

RC Senyamule aipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupata Hati safi

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MKOA wa Dodoma umeipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa hesabu zinazoishia tarehe 30 Juni, 2025. Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. “Mheshimiwa Naibu Meya, naomba nitumie nafasi hii kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa hesabu zinazoishia tarehe 30 Juni, 2025. Hati safi hii ya ukaguzi inaifanya halmashauri kuendelea kupata hati safi tangu mwaka 2017/2018 hadi sasa. Kitendo hiki kinaipa heshima kubwa halmashauri na mkoa kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya. Mafanikio haya makubwa yanatokana na ushirikiano wenu mkubwa waheshimiwa madiwani, watendaji wa jiji na viongozi mbalimbali. Hivyo, nawasihi kuendelea kudumish...