Posts

Showing posts from April 18, 2025

Shilingi Bilioni 7 zatekeleza miradi ya maendeleo Kata ya Miyuji

Image
Na. Coletha Charles, MIYUJI Diwani wa Kata ya Miyuji, Beatrice Ngerangera, ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni saba kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata yake na kusema kuwa miradi hiyo imebadilisha maisha ya wananchi na kuyafanya kuwa bora zaidi. Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Kata ya Miyuji kwa kipindi cha mwaka 2021-2025 na serikali. Alisema kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa miradi ya Kata ya Miyuji kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi. “Katika kipindi cha miaka minne, kata yetu ya Miyuji imenufaika na miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7. Hii ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari yenye miundombinu kamili kuanzia ‘O-Level’ hadi ‘A-Level’, ikiwa na mabweni na nyumba za walimu. Gharama yake ni shilingi 544,000,000 kutoka serikali kuu kupitia SEQUIP” alisema Diwani Ngerangera. ...

Waziri Mchengerwa atoa Maagizo mahususi kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi

Image
OR. TAMISEMI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mohamed Mchengerwa amewaelekeza wakuu wa mikoa kuwasimiamia Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia vipaumbele vya mwaka 2025/26 kikamilifu. Waziri Mchengerwa alitoa maelekezo hayo wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka 2025/26. Alisema kuwa vipaumbele vya kuzingatia ni kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafikia malengo na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya afya ya msingi, elimu ya msingi na sekondari kulingana na mipango iliyowekwa. Aidha, aliwataka kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidigitali ikiwemo uwekaji na matumizi ya mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na vituo vya huduma za afya na elimu. Vilevile, aliwaagiza kuhakikisha mapato katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa yanakusanywa kupitia mifumo ya TEHAMA ya serikali pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa...

TAMISEMI yakusanya Shilingi Trilioni 1.11

Image
OR-TAMISEMI WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema hadi kufikia Machi, 2025 shilingi trilioni 1.11 zimekusanywa sawa na asilimia 93.15 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.60 kwa Mwaka 2024/25. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2025/26, Waziri Mchengerwa alisema kuwa kati ya fedha hizo shilingi trilioni 61.21 ni kodi ya majengo, shilingi trilioni 1.04 ni mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa. Pia, alisema kuwa shilingi bilioni 16.23 ni mapato ya ndani ya taasisi na shilingi milioni 201.60 ni maduhuli ya mikoa. Alifafanua kuwa makusanyo hayo yalitokana na ada za wanachuo, tozo, ukusanyaji wa madeni, mauzo ya bidhaa mbalimbali na ushuru unaotozwa na mamlaka za serikali za mitaa kulingana na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290. Mchengerwa alisema kuwa kwa kipindi hicho, TAMISEMI ilipanga kutumia shilingi bilioni 541.27 za map...

Ujenzi wa Madarasa ya kisasa wavutia wanafunzi kusoma kwa bidii Sekondari Kikuyu

Image
Na. Leah Mabalwe, KIKUYU KASKAZINI    Mkuu wa Shule ya Sekondari Kikuyu, Mwl. Gasper Mmary amesema mradi wa ujenzi wa madarasa ya kisasa umekuwa chachu ya ufaulu na kuvutia wanafunzi kusoma kwa bidii. Alitoa kauli hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Kikuyu Kaskazini kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kutoa kiasi cha shilingi 40,000,000 kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya kisasa na ofisi moja ya walimu. “Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita, ujenzi huu wa madarasa ya kisasa umesaidia sana katika kupanda kwa taaluma kwa wanafunzi wetu na hata kupanda daraja la ufaulu. Madarasa haya yanawavutia wanafunzi kukaa kwa muda mrefu shuleni kwaajili ya kujisomea na mazingira kwa ujumla ni mazuri” alisema Mwl. Mmary. Kwa upande wake Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Kikuyu, Mwl. Mwajuma Kidela aliipongeza serikali kwa kujenga madarasa kwasababu yamelet...

Shule ya Sekondari Kikuyu yapongeza ajenda ya Lishe

Image
  Na. Abdul Juma, KIKUYU KASKAZINI Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha chakula na lishe linapatikana katika Shule ya Sekondari Kikuyu na kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa wameshiba. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kikuyu, Mwl. Gasper Mmary alipokuwa akiongelea hali ya upatikanaji wa chakula na lishe shuleni hapo yakiwa ni mafanikio ya serikali kwa miaka minne ya serikali. Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewezesha upatikanaji wa unga zaidi Kilogramu 650 ili kusaidia wanafunzi waliopo shuleni hapo kupata chakula shuleni. “Tunaushukuru mpango huu wa kuboresha chakula na lishe kwa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari. Katika mpango huu, halmashauri imetusaidia kupata unga zaidi ya Kilogramu 650 ili kuwezesha wanafunzi wote kupata chakula. Suala hili lina mchango mkubwa katika kuwafanya wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kupata ufaulu mzuri katika masomo yao” alisema Mwl. ...

Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

Image
Na. Coletha Charles, KIZOTA WANANCHI wa Kata ya Kizota, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wanufaika na mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kizota kilichogharimu kiasi cha shilingi 500,000,000.   Diwani wa Kata ya Kizota, Jamal Ngallya alisema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kilichogharimu kiasi cha shilingi milioni 500, kitaboresha kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kizota na maeneo Jirani. Kituo hicho kinachojumuisha majengo ya kisasa yenye uwezo wa kuhudumia mamia ya wananchi kwa siku na kuwaepushia kutembea umbali mrefu, alisema. Katika hatua nyingine aliongeza kuwa majengo yaliyojengwa katika kituo hicho ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la mionzi, jengo la huduma ya mama na mtoto, jengo la maabara, kichomea taka, na yataongezwa majengo mengine kama wodi za wagonjwa pamoja na jengo la kuhifadhia maiti. Alisema kuwa Kituo cha Afya Kizota ni miongoni mwa vituo vikubwa zaidi vya afya jijini Dodoma kwa sasa, na kinatarajiwa kuwa cha...

Miaka minne ya Dkt. Samia, Kizota yanufaika mikopo ya asilimia 10

Na. Coletha Charles, KIZOTA Wananchi wa Kata ya Kizota, Halmashauri ya Jiji la Dodoma waeleza kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa makundi ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, ikiwa ni hatua ya kuinua maisha yao kiuchumi na kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali.   Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Kizota, Theresia Ntui alipokuwa akiongelea mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita. Alisema kuwa tangu kuanza kwa utolewaji mikopo ya asilimia 10 katika awamu ya sita ya Rais, Dkt. Samia, Kata ya Kizota imenufaika kwa jumla ya shilingi 410,000,000 zilizotolewa kwa vikundi mbalimbali vya kijamii. Alisema kuwa katika fedha hizo, vikundi 28 vya wanawake vilipokea shilingi milioni 192, vikundi 16 vya vijana vilipewa shilingi milioni 164, na vikundi vitano vya watu wenye ulemavu vilipata shilingi milioni 49. “Mikopo hii ni yenye masharti nafuu, h...