Posts

Showing posts from February 16, 2025

Wananchi Makutupora wafunguka changamoto ya Maji, Umeme na Shule kwa Mkuu wa Mkoa

Na. Halima Majidi, DODOMA Wananchi wa Kata ya Makutupora, jijini Dodoma, wameeleza kilio chao juu ya changamoto kubwa zinazowakabili, zikiwemo ukosefu wa maji safi, matatizo ya umeme, pamoja na shule kuwa mbali, hali inayowakwamisha katika shughuli za kila siku. Wakizungumza katika mkutano wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika Kata ya Makutupora, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema wamekuwa wakikumbana na shida ya maji kwa muda mrefu, huku wakilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu. Akitoa kero hiyo, mkazi wa Mtaa wa Sekondari, Pasisi James, alisema kuwa, tangu kuhamia katika mtaa huo ni miaka mingi hivyo ameiomba serikali kuwasogezea huduma ya maji kwa sababu imekuwa ni changamoto kubwa na hivyo kushindwa kuendelea na kazi zao za kila siku. “Maji ni tatizo hapa kwetu, tunamiaka mingi tangu kuhamia hapa, nimekuja hata kusoma sijui mpaka leo bado tunahangaikia maji, tunachukua maji kwa wachina dumu moja hilo hilo ufulie pamoja na kunywa, hapo naomba mtusaidie” ...

Senyamule awasisitiza wanufaika wa TASAF kutumia pesa kujiletea maendeleo

Na. Aisha Ibrahim, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amewataka wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kutumia vizuri pesa wanayopewa na mfuko huo katika kufanyia shughuli mbalimbali za kuingiza kipato ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi katika jamii na taifa kwa ujumla. Aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara fupi ya kutembelea wanufaika wa Mfuko wa TASAF katika mtaa wa Mchemwa, Kata ya Makutupora, jijini Dodoma iliyokwenda na Kaulimbiu isemayo ‘TASAF, kwa pamoja tuondoe umaskini’. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, alisema kuwa miongoni mwa malengo ya TASAF ni kuhakikisha wanajamii wenye kipato cha chini wanainuka kiuchumi na kuwa na kipato cha juu ili kusaidia kuinua vipato vyao na familia zao kwa ujumla. “Mfuko wa TASAF umekuja ili kuwafanya wale wenye kipato cha chini kuongezeka na kuanza kupata kipato cha juu” alisema Senyamule. Katika hatua nyingine, aliwahimiza wanufaika wa mfuko huo kuipa thamani pesa hiyo kwa kufan...