TANESCO Ddodoma kuendelea kuboresha miundombinu ya umeme Jiji la Dodoma

Na. Mwandishi Wetu-DODOMA SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma limetoa semina kwa madiwani wa kata zote 41 za Jiji la Dodoma lengo likiwa ni kueleza mikakati ya shirika hilo pamoja na miradi inayotekelezwa katika Mkoa wa Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Madiwani, kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya na Polisi kata wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ulioandaliwa na Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Dodoma Akitoa elimu jijini Dodoma, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Donasiano Shamba alisema kikao hicho kimejumuisha Madiwani, Kamati ya Usalama Wilaya na Polisi kata wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Kikao hiki kimehusisha madiwani kutoka kata zote 41 za Jiji la Dodoma pamoja na Polisi kata lengo ni kueleza mikakati yetu lakini pia kueleza changamoto zinazotukabili sisi kama shirika hasa suala la uharibifu wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme” alisema Mhandisi Shamba...