Posts

Showing posts from November 10, 2026

Hombolo kuanza safari ya kujengwa kwa mji mpya wa kisasa

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA   Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeingia hatua nyingine ya kuimarisha maendeleo ya mji mkuu wa nchi baada ya kusaini mkataba wa upembuzi yakinifu na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC). Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alisema kuwa mradi huo ni hatua muhimu katika utekelezaji wa dira ya kulifanya Dodoma kuwa jiji la kisasa lenye hadhi na viwango vya kimataifa. Alisema kuwa mkandarasi ameeleza uwezo wa kukamilisha kazi hiyo ndani ya kipindi kifupi, endapo atapata ushirikiano unaohitajika kutoka kwa viongozi, wataalamu na wadau wote wanaohusika na mradi. Shekimweri aliipongeza Serikali kwa kuendeleza azma ya kuijenga Dodoma, akisema mradi huo unaakisi dhamira ya kuongeza uwekezaji katika miundombinu na kuimarisha hadhi ya makao makuu ya nchi. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kushirikisha wananchi, sekta binafsi na wataalamu wa ardhi katika maandalizi ya mradi, ili kulinda mip...

Wananchi wa Hombolo wafurahia ujio wa mji wa kisasa

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Wananchi wa Kata ya Hombolo, jijini Dodoma, wameeleza matumaini makubwa kuhusu Mradi wa Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC), wakiamini kuwa utachochea ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira na kuharakisha maendeleo ya eneo hilo.   Wakizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa Mpango Kabambe wa HOTSAC, iliyofanyika Chinangali Park, Kata ya Chamwino, wananchi hao walisema wanatarajia kunufaika na fursa zitakazotokana na mradi huo. Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani, Asedi Ndajiro alisema kuwa wananchi wamekuwa na matarajio makubwa ya mradi huo kwa muda mrefu, wakiamini kuwa utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili. Alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kufungua fursa za ajira na kuharakisha maendeleo ya eneo hilo, huku wananchi wakisubiri kwa hamu kuanza kwa utekelezaji wake. Aliongeza kuwa ni muhimu wananchi washirikishwe katika utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kunufaika na...

DC Shekimweri ataka wananchi washirikishwe katika ujenzi wa Mji wa Kisasa Hombolo

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Wananchi, sekta binafsi na makundi mbalimbali wametakiwa kushirikishwa katika maandalizi ya Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC), ili wanufaike na fursa za kiuchumi zitakazotokana na mradi huo. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabiri Shekimweri, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa upembuzi yakinifu na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Hombolo, Chinangali Park, jijini Dodoma. Alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kufungua fursa za ajira, biashara, ujenzi, viwanda na huduma, hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa mapema kuzitumia fursa hizo wakati wa utekelezaji na baada ya kukamilika. Alisisitiza kuwa umuhimu wa kuandaa mpango wa usimamizi wa wadau na kushirikisha wataalamu wa ardhi ili kudhibiti matumizi yasiyopangwa, kuzuia migogoro na kuhakikisha maendeleo yanazingatia Mpango Kabambe wa Hombolo.   Kwa upande wake, Mkazi wa Kata ya Hombolo Makulu, Jiji la Dodoma Agness Matiko alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kuleta maendeleo kw...

Hombolo Satellite City kuibadilisha Dodoma, mradi wa mji wa kisasa wachukua sura mpya

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Jiji la Dodoma linatarajia kupata sura mpya kupitia mradi wa Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC), kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa upembuzi yakinifu na uandaaji wa Mpango Kabambe. Mkataba huo umesainiwa Chinangali Park, Kata ya Chamwino, jijini Dodoma, katika hafla iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa, viongozi mbalimbali, wawekezaji na wawakilishi wa taasisi za umma na binafsi. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alisema kuwa utekelezaji wa mpango huo utakuwa chachu ya mabadiliko makubwa yatakayoiwezesha Dodoma kuendana na hadhi yake kama makao makuu ya nchi. Alisema kuwa maandalizi yaliyoanza mwishoni mwa mwaka 2024 yalihusisha tafiti na ziara za mafunzo katika mataifa mbalimbali, ikiwemo Korea, hatua iliyoongeza uelewa na uwezo wa wataalamu wa ndani. Alisema kuwa sekta binafsi itakuwa mhimili wa utekelezaji, huku taasisi za fedha zikionesha mwitikio mkubwa wa kushiriki katika uwekezaji na kufadhili fursa zitakazotokana na mpango huo. Kw...

Dodoma yaweka historia kwa utiaji saini mkataba wa huduma za ushauri elekezi kidigitali

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Halmshauri ya Jiji la Dodoma na Kampuni ya Heerim Architects & Planners ya Korea Kusini zimesaini mkataba wa upembuzi yakinifu na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC). Utiaji saini huo umefanyika Chinangali Park, Kata ya Chamwino, jijini Dodoma, kwa njia ya kidijitali, ukiashiria hatua mpya katika matumizi ya teknolojia kwenye shughuli za kiutawala na miradi ya maendeleo. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alisema kuwa utaratibu huo unaonesha mabadiliko kutoka matumizi ya nyaraka za karatasi kwenda mifumo ya kidijitali, kwa kuzingatia matakwa ya sheria kikamilifu. Alisema kuwa maandalizi ya mradi yalihusisha tafiti na ziara za mafunzo katika nchi mbalimbali, zilizolenga kuongeza uwezo wa wataalamu wa ndani kutoa ushauri na kushiriki kikamilifu katika uandaaji wa mpango mpya. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Heerim Architects & Planners, Young Kyoon Jeong alisema kuwa kampuni hiyo italeta utaalamu na...

Mfumo wa NeST warahisisha utiaji saini mkataba wa HOTSAC, Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Mfumo wa kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NeST) umerahisisha utiaji saini wa mkataba wa upembuzi yakinifu na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC), jijini Dodoma. Akizungumzia zoezi la kusaini kidigitali mkataba huo, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Vincent Odero alisema kuwa mfumo huo umewezesha mchakato mzima kufanyika kwa uwazi, haki na bila upendeleo. Alisema kuwa mchakato wa kumpata mtaalamu mshauri ulifanyika kupitia mfumo wa NeST, kuanzia hatua ya kutangaza zabuni, kufanya tathmini, majadiliano, upekuzi wa mkataba kwa Mwanasheria mkuu wa serikali hadi kukamilisha na kusaini mkataba. Alieleza kuwa mtaalamu mshauri aliyepatikana ni kampuni ya heerim architects & planners kutoka Korea Kusini, kwa kushirikiana na kampuni ya ndani Arm City Consultants itakayotekeleza majukumu kama Mshauri msaidizi. Aliongeza kuwa mkataba unahifadhiwa ndani ya mfumo wa NeST, hivyo kurahisisha upatikanaji wake wakati wowote unapohitajika,...