Posts

Showing posts from September 16, 2023

WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGIZI NDOGO WA DIWANI KATA YA NALA WAASWA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WASIMAMIZI wa vituo vya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala wametakiwa kufanya kazi kwa nidhami, hekima na uzalendo na kuepuka kuisababishia serikali hasara. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo akiwaapisha wasimamizi wa vituo vya uchaguzi mdogo Kata ya Nala Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi kwenye vituo vya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala, Jimbo la Dodoma mjini yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma. Kayombo ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “niwaombe sana wasimamizi wa vituo, uchaguzi ni suala nyeti sana sikiliza kwa makini maelekezo ya viongozi na fuata taratibu na sheria zilizopo, ukikosea utaitia serikali katika hasara kubwa. Kuweni na nidhamu, hekima na uzalendo kwa kiwango cha juu sana. Baadhi yenu mlishasimamia chaguzi nyingi ila uchaguzi hauhitaji mazoe...