Posts

Showing posts from July 3, 2024

Kituo cha Afya Ilazo kuhudumia wananchi zaidi ya 99,000 Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI MRADI wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo utakapokamilika utahudumia wananchi 99,743 wa Kata ya Nzuguni na maeneo ya jirani ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Muonekano wa juu wa Kituo cha Afya Ilazo Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024. Dkt. Method alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha huduma za mama na mtoto na huduma za upasuaji ukitarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 99,743 wa Kata ya Nzuguni, Ipagala na maeneo menginge watapata huduma bora za afya mradi huo utakapokamilika. Akiongelea mafanikio ya mradi huo, aliyataja kuwa ni kuwezesha kutoa huduma za upasuaji, kliniki ya mama na mtoto, huduma za kujifungua, wodi ya watoto wachanga , huduma za kuhifadhi miili. Mafanikio me...

Mtendaji Kata Nkuhungu anena fursa kongamano la vijana

Image
Na. Dennis Gondwe, NKUHUNGU Kongamano la vijana ni fursa ya kuwakutanisha vijana wa Kata ya Nkuhungu na wenzao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Dodoma kujadili fursa zilizopo na jinsi ya kuzifikia kwa ajili ya kujiletea maendeleo. Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkuhungu, Mwasiti Migilla akiwa katika moja ya majukumu yake Baadhi ya washiriki wa kongamano la vijana Wilaya ya Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkuhungu, Mwasiti Migilla alipokuwa akiwapokea vijana wanaohuduria kongamano la vijana linalofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Nkuhungu jijini Dodoma likienda sambamba na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 wilayani Dodoma. Migilla  alisema kuwa kata yake imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa kongamano la vijana na mkesha wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 katika Wilaya ya Dodoma. “Matukio haya mawili ni makubwa na ni heshima kubwa kwetu wananchi wa Kata ya Nkuhungu. Vijana wanapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu pamoja na kujadili fursa mbali...

Mwenge wa Uhuru 2024 kutembelea miradi ya Bil. 7 Wilaya ya Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA MWENGE wa Uhuru mwaka 2024 utatembelea, kuzindua na kuweka jiwe la msingi jumla ya miradi saba yenye thamani ya shilingi 7,096,668,714.32 wilayani Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabi Shekimweri (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongela (kulia) leo katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari John Merlin Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongela mapema leo katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari John Merlin iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema “ninakiri kwa dhati ya moyo wangu kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwako Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongela. Aidha, ninakiri kumpokea Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Godfrey Mnzava pamoja na wenzake watano. Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Dodoma utatembelea miradi saba yenye jumla ya ...

Dodoma English Medium imewasaidia wazazi wa kipato cha kati kusomesha

Image
Na. Dennis Gondwe, IPAGALA MRADI wa ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi Dodoma English Medium umewasaidia wazazi wenye kipato cha kati kusomesha watoto wao katika shule ya mchepuo wa kiingereza karibu na maeneo yao kwa gharama nafuu. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prisca Myalla alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Dodoma English Medium kwa Kiogozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024. Akiongelea faida za mradi huo alizitaja kuwa ni kuwasaidia wazazi wenye kipato cha kati kupata fursa ya kusomesha watoto kwenye shule ya mchepuo wa ki i ngereza . Faida nyingine aliitaja kuwa ni wananchi kusogezewa huduma ya shule karibu ambapo watoto walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma ya elimu pia wanafunzi wanapata elimu bora kwa gharama nafuu ukilinganisha na shule binafsi . “ Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, m radi umelenga kutoa elimu bora am...

Bagamoyo Garden yaajiri vijana 20 Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe MRADI wa Bagamoyo Garden wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, maua na nyasi unalenga kuunga mkono juhudi za serikali za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani na inayopendeza. Sehemu ya muonekano wa Bagamoyo Garden Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa mradi wa Bagamoyo Garden, Rogasian Malya alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa Bagamoyo Garden wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, maua na nyasi katika eneo la wazi kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024. Malya alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuunga mkono juhudi za s erikali za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa njia ya upandaji miti , k ampeni ambayo ilizinduliwa mwaka 2021 kwa kupanda miti katika chanzo cha maji Mzakwe na aliyekuwa Makamu wa Rais ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe shimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alisema kuwa m radi hu o unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa m bio za Mwenge wa Uhuru, 2024 use...

Mwenge wa Uhuru 2024 waweka jiwe la msingi Kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group

Image
  Na. Dennis Gondwe, MIYUJI KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi na kupongeza uwekezaji uliofanywa na Dodoma Media Group baada ya kutembelea na kukagua kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group kilichojengwa eneo la Miyuji. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mnzava baada ya kuweka jiwe la msingi kituo cha vyombo vya habari Dodoma Media Group Mnzava baada ya kutembelea, kukagua na kujiridhisha na uwekezaji huo alipongeza na kusema kuwa ni uwekezaji mkubwa na mzuri. Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri kwa uwekezaji wa sekta binafsi nchini. Mazingira ya ufanyaji kazi kwa vyombo binafsi vya habari yameboreshwa katika kipindi chake, aliongeza. Aidha, aliweka jiwe la msingi mradi wa kituo cha vyombo vya Habari cha Dodoma Media Group. Akiongelea gharama za mradi huo, meneja mkuu, Zania Miraji alisema kuwa hadi kukamil...

Dodoma Media Group

Image
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI Kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group kutoa elimu ya mpiga kura katika kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na utunzaji wa mazingira. Mejena Mkuu wa Dodoma Media Group, Zania Miraji alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group Kauli hiyo ilitolewa na Mejena Mkuu wa Dodoma Media Group, Zania Miraji alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group kilichopo katika Mtaa wa Miyuji Proper jijini Dodoma kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024. Miraji alisema “ kupitia vyombo vya habari vya Dodoma Media Group jamii ya Dodoma itapata haki ya upatikanaji wa taarifa na elimu juu ya masuala mbalimbali ikizingatia ujumbe wa ‘ Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa E ndelevu ’ . Elimu itakayotolewa ni pamoja na elimu ya masuala ya uchaguzi ikiwemo elimu ya mpiga kura ambapo kutakuwa na kipindi maalum cha kueli...