JAMII DODOMA YASHAURIWA KUSAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM
Na. Dennis Gondwe, HOMBOLO BWAWANI JAMII imeshauriwa kutenga muda kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili waweze kujimudu na kufikia malengo ambayo taifa linapenda. Mdau wa elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Tatu Mwangu akimpatia zawadi mtoto Kauli hiyo ilitolewa na mdau wa elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Tatu Mwangu alipoungana na Jumuiya ya Shule ya Msingi Feza tawi la Dodoma kutoa msaada wa viti mwendo nane na vifaa vya elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Hombolo Bwawani. Mwl. Mwangu alisema “katika hali ya kawaida sisi kama jamii tunawajibika kuwasaidia wote wasio na uhitaji na wenye uhitaji maalum kufikia ndoto zao. Leo kupitia familia ya Shule ya Feza wamepewa vifaa vya kuwasaidia katika kujifunza na kuweza kutembea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa wale wenye changamoto ya viungo. Tuishukuru familia ya Shule ya Feza kwa kutushirikisha wazazi. Kwa kufanya hi...