Jiji la Dodoma lawapa vijana fursa mikopo ya 10%
Na. Mwandishi wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10, hatua inayowapa nafasi ya kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za uzalishaji, ikiwemo viwanda vidogo, utengenezaji wa bidhaa na utunzaji wa mazingira. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale, Husna Toni mara baada ya kutembelea vikundi vya vijana vinavyofanya shughuli mbalimbali katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa ziara hiyo imetoa fursa ya kujifunza namna vijana wa Jiji la Dodoma wanavyotumia mikopo ya asilimia 10 kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya jamii. “Vijana wa Dodoma wana uthubutu mkubwa katika shughuli za uzalishaji, viwanda na utunzaji wa mazingira. Hii inatuonesha kwamba fursa zipo na vijana wakipewa mitaji na mazingira mazuri wanaweza kujiajiri na kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa” alisema Toni. Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kutumia fursa zinazopatikana, husus...