Posts

Showing posts from February 15, 2024

JIJI LA Dodoma linajali wanafunzi

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inawaonea huruma na kuwajali wanafunzi kwa watengenezea mazingira mazuri ya kujifunzia. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la Diwani wa Hazina, Samwel Mziba aliyetaka kujua ni lini halmashauri itakuwa na huruma kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru kwa kuifanyia ukarabati mkubwa ili iendane na hadhi ya jiji. Fungo alisema kuwa halmashauri inawaonea huruma wanafunzi na kuwajali kwa wajengea miundombinu ili waweze kusoma katika mazingira bora na salama. “Mheshimiwa mwenyekiti, tulimpeleka mhandisi kufanya makadirio ya gharama za kufanya ukarabati wa madarasa yaliyochakaa katika shule hiyo na mipaka kwa ajili ya ujenzi wa uzio. Hadi sasa mbao na ‘gypsum board’ zimeshafika shuleni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa shule hiyo” alisema Fungo. Aidha, Mstahiki Meya alisema kuwa kuna utayari ...

Mchakato kugawa mitaa kuanzia kwenye mitaa

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wametaarifiwa kuwa mchakato wa kugawa maeneo ya mitaa ambayo yanaonekana makubwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo akijibu maswali ya papo kwa papo Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Diwani wa Kata ya Iyumbu, Richard Sutuchi aliyetaka kujua utaratibu wa wa kugawa maeneo ya mitaa ili kusogeza huduma kwa wananchi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Fungo, alisema kuwa utaratibu wa kugawa mitaa unaanzia katika mitaa husika. “Mapendekezo yanatoka katika mitaa husika na utaratibu huo unapelekwa katika kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hadi halmashauri. Hivyo, mchakato uanzie kwenye mtaa” alisema Fungo. MWISHO

Dodoma Sec yateuliwa ufundishaji mubashara nchini

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limetaarifiwa kuwa Shule ya Sekondari Dodoma imeteuliwa kuwa miongoni mwa shule 10 za majaribio ya ufundishaji mubashara nchini. Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe akisisitiza jambo Taarifa hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akitoa taarifa ya Mwenyekiti katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Prof. Mwamfupe alisema kuwa Shule ya Sekondari Dodoma imeteuliwa kuwa miongoni mwa shule 10 za majaribio nchini ya ufundishaji mubashara kwa njia ya mtandao. Alisema kuwa ufundishaji huo unamuwezesha mwalimu wa shule moja kufundisha idadi kubwa ya shule kadri inavyowezesha. “Mwalimu yupo Shule ya Sekondari Kibaha anafundisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma na wanafunzi wote wanamuona na wanapata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa. Gharama ya mtambo...