Posts
Showing posts from July 2, 2024
Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Dodoma vyapongezwa kwa utendaji kazi mzuri
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA VITENGO vya Mawasiliano Serikalini katika Mkoa wa Dodoma vimepongezwa kwa kuhabarisha wananchi juu ya kazi nzuri zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya Mkoa wa Dodoma kushika nafasi ya nne katika utoaji habari nchini kufuatia tathimini iliyofanywa na Idara ya Habari (Maelezo) chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari juu ya umahili wa utoaji habari kwa vitengo vya mawasiliano serikalini. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya wakati akipokea zawadi ya kikombe na cheti baada ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kushika nafasi ya nne kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara. Mmuya alisema “napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kuhabarisha wananchi juu ya kazi na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Dodoma. Hakika mmemuheshimisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule. Nimefahamishwa kuwa...