SERIKALI YAANZISHA KLINIKI YA ARDHI DODOMA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Na. Dennis Gondwe, DODOMA SERIKALI imeanzisha kliniki maalum ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya awamu ya sita. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu alipotembelea siku ya kwanza ya utekelezaji wa majukumu ya kliniki hiyo na kuongea na mamia ya wananchi waliojitokeza katika eneo la iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya zamani jijini hapa. Gugu alisema “hii ni kliniki maalum ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akishirikiana na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma na Katibu Tawala Msaidizi anayehusika na Miundombinu akiiwakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Lengo ni kuwasikiliza na kutambua kero zenu kwenye masuala ya Ardhi katika Jiji la Dodoma. Tumekuja kuwasilikiza tutambue kero zenu na wananchi wanaotaka kuhakiki maeneo yao na hati miliki tuweze kuwapatia”. Alisema kuwa kliniki hiyo inaashiria dhamira y...