Posts

Showing posts from May 28, 2025

Shilingi Milioni 473 kutekeleza Mradi wa Ufungaji CCTV Kamera Jiji la Dodoma

Image
Na. Josephina Kayugwa, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesani mkataba na Kampuni ya Wisjane Smart Systems kwaajili ya ufungaji wa kamera za usalama barabarani (CCTV) unaogharimu shilingi 473,000,000 ikiwa ni mradi utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu. Akitoa taarifa ya mradi, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alisema kuwa mradi huo utakwenda kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Dodoma kwasababu kamera hizo zitafanya kazi masaa 24. “Mradi huu wa gharama ya shilingi 473,000,000 utahusisha ufungaji wa kamera kwenye barabara zinazoinga njia kuu lakini pia hapo baadae utakuja kuimarishwa zaidi kwa kuongeza sehemu nyingine za kuweka kamera lengo ni kupata picha zote za vyombo vya usafiri vitakavyokuwa vikiingia na kutoka katika Jiji la Dodoma” alisema Fungo. Aliongeza kuwa wana mpango wa kuunganisha mfumo huo na taasisi nyingine ili kuimarisha ulinzi na usalama. “Mfumo huu baada ya muda tuta...