Ujenzi Ofisi Kata Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati
Na. Leah Mabalwe, MBALAWALA Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi. Hayo yalizungumzwa na Mhandisi wa Jiji la Dodoma, Mhandisi Ally Bella, katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala robo ya tatu 2024/2025 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema “ninakuagiza Afisa Mtendaji wa kata hii ya Mbalawala kusimamia mradi huu uweze kukamilika kwa haraka kwasababu wananchi wa eneo hili wanategemea ofisi hii kwaajili ya kupata huduma” alisema Mhandisi Bella. Nae, Awadhi Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. “Binafsi niishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, kwasababu kazi za maendeleo zinaendelea kufanyika katika kila maeneno na sehemu ambazo hakuna basi Jiji la Dodoma...