Lishe bora yahamasishwa Kliniki ya Magonjwa Yasiyoambukiza Nyerere Square
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mamia ya wananchi wamejitokeza kupima afya zao katika kliniki maalum ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuongeza uelewa kuhusu uchunguzi wa mapema, lishe bora na kuzuia magonjwa yanayoendelea kuongezeka nchini. Taarifa hiyo ilitolewa na Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii, Dr. Peter Daud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika bustani ya mapumziko Nyerere Square ambapo maadhimisho ya wiki ya Upimaji Magonjwa yasiyoambukiza yakitamatika. Dr. Daud alisema kuwa mwamko mkubwa ulioonekana ni ishara kuwa elimu ya lishe na uchunguzi wa mapema inawafikia wananchi kwa ufanisi. “Sehemu kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza inahusiana na lishe. Tunawahimiza wananchi kupunguza vyakula vyenye mafuta mengi, kula kwa uwiano sahihi na kufanya mazoezi. Hii ni kinga muhimu sana” alisema Dr. Daud. Aliongeza kwa kutoa wito kuwa wananchi waache tabia bwete kwa kuhakikisha wanafanya mazoezi, kutembea umbali mdogo kwaajili ya kuweka mwili na misuli t...