Posts

Showing posts from October 5, 2026

Watoa huduma wapatiwa mafunzo ya Lishe kwa wajawazito

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Watoa huduma za afya wanaohudumia wajawazito katika kliniki za huduma za mama na mtoto (ANC) wamepatiwa mafunzo kuhusu utekelezaji wa utafiti unaolenga kuboresha huduma za lishe kwa wajawazito katika Jiji la Dodoma. Mafunzo hayo yalijikita katika kuwaongezea uwezo watoa huduma kuhusu utoaji wa elimu na huduma za lishe kwa wajawazito, ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa damu wakati wa ujauzito. Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Victor Kweka aliwataka watoa huduma kutumia maarifa wanayoyapata katika mafunzo hayo katika kuboresha huduma zinazotolewa kwa wajawazito katika vituo vya afya. “Utoaji wa elimu sahihi kuhusu lishe na matumizi ya virutubisho vya nyongeza ni sehemu muhimu ya kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora na salama katika kipindi chote cha ujauzito, hivyo mnatakiwa kuhakikisha kila mjamzito anapokuja kliniki anapewa elimu ya lishe na umuhimu wa kunywa dawa” alisema Kweka. Kw...