Wanawake watakiwa kujitathmini katika uongozi
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wanawake watakiwa kujitathmini katika nyanja za uongozi kwa kuonesha nia ya kuwajibika ipasavyo na kuchangamkia fursa za uongozi zinazojitokeza katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akizungumza na maelfu ya wanawake waliojitokeza katika kongamano la kanda ya kati lililohusisha mikoa mitatu (Dodoma, Singida na Iringa) katika kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma. Senyamule alisema ānaomba nitoe shime kila mmoja wetu ajitathmini hatua gani amechukua kuonesha uwezo wake wa kuongoza katika eneo alilopewa. Ni imani yangu kuwa kila mahali tunatosha kwasababu Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha uwezo wa kutosha kwenye nafasi ya urais. Kwahiyo, wanawake tunaweza katika kila eneoā. Akiongelea kuhusu takwimu za wanawake viongozi wa Mkoa wa Dodoma, alisema karibu ngazi zote za uongozi kuna viongozi wa kike na takwimu z...