Posts
Showing posts from July 19, 2023
Waziri Mkuu Mgeni Rasmi NBC Dodoma Marathon 2023
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma

Dodoma, Julai 19, 2023 – Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2023 zinazotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 23 Julai 2023. Mbio za mwaka huu zinalenga kukusanya jumla ya shilingi milioni 500. Fedha hizo zitatumika kusaidia kupambana na kansa ya shingo ya kizazi pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wakunga ikiwa ni sehemu ya kusaidia kuongeza wataalamu ili kupunguza vifo vya uzazi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya mbio hizo zilizojizolea umaarufu mkubwa na ambazo zinafanyika kwa mara ya nne mfululizo mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alisema mkoa umejipanga vyema kuwapokea wakiambiaji na wageni wote wataoshiriki. “Kwanza kabisa napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kuandaa mbio hizi zenye faida kubwa kwetu kama nchi. Pili niwahakikishie washiriki wote kuwa sisi kama mkoa wa Dodoma tumejipanga vy...
WAAJIRIWA SEKTA BINAFSI WATAKIWA KUZINGATIA KIMA KIPYA CHA MSHAHARA
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
.jpg)
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma OFISI ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi imewataka waajiri wa sekta binafsi nchini kuzingatia kima kipya cha chini cha mshahara kilichotangazwa na serikali mwaka huu kwa kuwa ni takwa la kisheria. Kamishna wa Kazi Msaidizi anayeshughulikia Mahusiano kazini Bw. Andrew Mwalwisi akitoa elimu kwa umma jijini Dodoma kuhusu sheria na miongozo ya kazi Kima hicho kilitangazwa katika kupitia tangazo la serikali namba 687 na kilianza kutumia Januari mosi, 2023 na kimewekwa kwenye sekta kuu 13. Kamishna wa Kazi Msaidizi, Mahusiano kazini wa Ofisi hiyo, Andrew Mwalwisi ameyasema hayo Julai 19, 2023 alipokuwa akitoa elimu kwa umma jijini Dodoma kuhusu sheria na miongozo ya kazi. Amesema kwa sekta ya kilimo ni Sh.140,000, afya (Sh.195,000), mawasiliano imegawanyika kuna sekta ya huduma za mawasiliano (Sh.500,000), huduma za utangazaji na vyombo vya habari, posta usafirishaji vifurushi ...
KAMATI YA FEDHA JIJI LA DODOMA YATEMBELEA KIKUNDI CHA NASHA
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Naibu Waziri Nderiananga ateta na Wanafunzi wa Weruweru
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
.jpeg)
Na. Mwandishi Wetu- Moshi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga awaasa vijana kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kuyafikia malengo waliyonayo. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Weruweru alipowatembelea shule hiyo Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Weruweru alipotembelea mapema Julai 16, 2023 shuleni hapo kwa lengo la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule hiyo ambayo aliwahi kusoma na kutoa zawadi za taulo za kike na mafuta ya ngozi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa uongozi wa shule hiyo. Mhe. Nderiananga aliwaeleza upo umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari za masuala yanayohusu Virusi vya UKIMWI kwani kwa mujibu wa tafiti za viashiria vya VVU na UKIMIWI mwaka 2016/17 zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya maambukizi ipo kwa vijana mweny...