Prof. Mohamed ahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwapongeza wazazi
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makutupora watakiwa kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao ya kielimu na maisha kwa ujumla. Hayo aliyasema Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania, Prof. Said Mohamed wakati wa Uzinduzi wa Upandaji Miti mwaka 2025/2026 uliofanyika katika Shule ya Sekondari Makutupora Jijini Dodoma. Alisema kuwa juhudi za wanafunzi katika masomo ni msingi muhimu wa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla. “Msingi mzuri wa watoto ni kupata elimu hivyo niwasihi wanafunzi muendelee kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia ndoto zenu, kwasababu hapa kuna viongozi wa baadae ambao wataweza kuongoza taifa letu, lakini pia muwe na nidhamu kwasababu nidhamu ndio hupelekea kufika mbali hususan katika masomo yenu” alisema Prof. Mohamed. Aidha aliwapongeza wazazi kwa juhudi wanazozifanya katika malezi ya watoto. “Nipende kuwapongeza wazazi kwa namna ambavyo mnaendelea kuwalea watoto katika misingi bora, lakini pia nisisitize u...