Makamu wa Rais azungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Philip Mpango ameiagiza Serikali ngazi ya Mkoa wa Dodoma kuendelea kutafutia ufumbuzi migogoro ya ardhi iliyokithiri hususan fidia kwa ardhi iliyotwaliwa na utekelezaji wa mgawanyo wa ardhi wa 70% kwa 30%. Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma katika Mkutano uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amesema changamoto hiyo ya ardhi mkoani Dodoma kwa kiasi kikubwa imewafanya wanachama pamoja na wananchi kuwa na manung’uniko na hata kufikia hatua ya kususia uchaguzi. Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kushirikiana na Waziri wa Ardhi kwa pamoja na uongozi wa Jiji la Dodoma kuongeza nguvu zaidi katika kushughulikia migogoro hiyo. Dkt. Mpango amewahimiza viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani ...