Dkt. Sagamiko asema, ugawaji jimbo hauna athari kwa huduma zinazotolewa na Jiji la Dodoma
Na, Nancy Kivuyo, DODOMA Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alitoa hofu Baraza la Madiwani kuwa kukidhi vigezo vya ugawaji wa Jimbo la Dodoma Mjini hauna athari katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika kuwahudumia wananchi. Aliyasema hayo wakati akijibu hoja za madiwani waliohudhuria katika Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa ya mapendekezo ya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. āMgawanyo wa jimbo kwa upande wa tarafa hauna kikwazo chochote, kama ni kata ni kikwazo kwasababu kata moja haiwezi kuwa katika majimbo mawili. Leo tutaangalia zaidi kwenye kataā alisema Dkt. Sagamiko. Aliongeza kuwa, athari za mgawanyo wa jimbo kimapato unalenga mgawanyo wa majimbo na sio shughuli za kiutendaji. āNiwatoe wasiwasi, utoaji wa huduma kwa wananchi utaendelea kama ilivyokua awali na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Baraza litakua moja bila kujali jimbo analotoka diwani. M...