RC Dodoma aongoza zoezi la upandaji Miti Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma wajitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupanda miti katika maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Zoerzi hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika Kata ya Makutupora. ZOezi hilo linatarajia kupanda miti takribani 100,000. Miti hiyo inapandwa jirani na barabara ya mzunguko (ring road). Tukio hilo pamoja na mkuu wa mkoa aliambanata na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, wakuu wa Divisheni na Vitengo, maafisa waandamizi kutoka serikalini na taasisi binafsi na wamia ya wananchi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akipanda mti