Posts

Showing posts from October 29, 2024

Wanawake Jiji la Dodoma washauriwa kuandaa vyakula kwa nishati safi ya kupikia

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wanawake wameshauriwa kutumia nishati safi ya kupikia katika kuandaa vyakula vya watoto kwasababu upatikanaji wake ni rahisi ukilinganisha na matumizi ya nishati chafu ya kupikia kama vile mkaa na kuni kutokana na kuwa inaokoa muda na ni salama kwa mazingira. Afisa Lishe wa Kituo cha Afya cha Makole, Frida Mollel wakati akitoa mafunzo kwa vitendo juu ya jiko darasa kwa akina mama wanaonyonyesha waliohudhuria kliniki Ushauri huo ulitolewa na Afisa Lishe wa Kituo cha Afya cha Makole, Frida Mollel wakati akiwafundisha juu ya jiko darasa kwa akina mama wanaonyonyesha waliohudhuria kliniki katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mollel aliwataka kutumia nishati safi ya kupikia wanapoandaa chakula cha watoto wao kwasababu upatikanaji wake ni rahisi na usalama kwa mtoto ni mkubwa zaidi ukilinganisha na matumizi ya nishati chafu ya kupikia. “Sambamba na elimu ambayo tumeitoa, utumiaji wa nishati safi umekuwa ukirahisisha uandaaji wa ...

Elimu ya unyonyeshaji sahihi yatolewa kwa kina mama Jiji la Dodoma

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Akina mama wamepewa elimu ya unyonyeshaji sahihi maziwa ya mama kwa lengo la kuwajengea uelewa mpana utakaowasaidia kuwakuza vizuri watoto wao ili wawe na afya njema na lishe bora katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Afisa Muuguzi Msaidizi, Kituo cha Afya Makole, Christopher Tarimo akielezea njia sahihi ya kumshika mtoto wakati wa kumnyonyesha maziwa ya mama Hayo yalisemwa na Afisa Muuguzi Msaidizi, Kituo cha Afya Makole, Christopher Tarimo, alipokuwa akitoa elimu ya namna sahihi ya kumnyonyesha mtoto na lishe kwa akina mama waliojifungua katika wodi ya wazazi kituoni hapo. Akizungumza na akina mama hao Afisa Muuguzi Msaizidi, aliwashauri kuzingatia mikao ya unyonyeshaji pindi wanapowanyonyesha watoto wao. “Katika unyonyeshaji lazima tutenge muda, ile nusu saa ya kwanza au lisaa limoja hakikisha kwamba simu umeweka pembeni, hausumbuliwi na mtu yeyote unakuwa umetulia mawazo yote kwa mtoto. Unatakiwa uwe umekaa, tunashauri sana kumnyonyesha mtoto ukiwa um...

Jiji la Dodoma kukusanya shilingi 1,902,895,000.00 kutoka Soko la wazi la Machinga

Image
  Na. Asteria Frank, DODOMA   Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 1,902,895,000.00 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko la wazi la Machinga ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.   Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko wakati akisoma taarifa ya uendeshaji wa Soko la wazi la Machinga kwa Kamati kudumu ya Bunge ya Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya soko hilo lililopo eneo la Bahi Road jijini Dodoma.   Dkt. Sagamiko alisema kuwa ujenzi wa soko hilo uligharimu kiasi cha shilingi 9,529,747,200.66. Kati ya fedha hizo shilingi 6,529,747,200.66 ni mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji, shilingi 2,500,000,000.00 ni ruzuku kutoka Serikali kuu na shilingi 500,000,00.00 ni fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ...