BEST WESTERN DODOMA CITY HOTEL SULUHU MALAZI MAKAO MAKUU

Na. Dennis Gondwe, DODOMA Ujenzi wa Hoteli ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma umeitikia changamoto ya huduma ya malazi kwa mabalozi na wageni wengine wanaotembelea makao makuu ya nchi kwa huduma mbalimbali. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilipotembea miradi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Senyamule alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inakabiliwa na changamoto ya sehemu za malazi kwa mabalozi na wageni mashuhuri. “Kuwepo kwa vitega uchumi hivi Jengo la Kitega Uchumi Mtumba na Hoteli ya Best Western Dodoma City ni faida kubwa wa maendeleo ya Dodoma. Mheshimiwa Mwenyekiti mabalozi wengi walikuwa wanakuja Dodoma na kurudi Dar es Salaam, Balozi anakuja na ndege ya asubuhi anaenda wizarani akimaliza shughuli zilizompeleka anaondoka. Sasa hivi mabalozi wengi wanafikia Best Western Dodoma City Ho...