Jiji la Dodoma lafikisha 93% ya ukusanyaji Mapato

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufikia asilimia 93 ya makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2025 na kusema kuwa ukusanyaji huo unatoa matumaini ya kufikia lengo ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha.



Pongezi hizo alizitoa katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.


Senyamule alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya uchambuzi wa mapato ya mamlaka za serikali za mitaa kwa Mkoa wa Dodoma uliofanywa na wataalam wa ofisi yake hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2025 Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilikuwa imekusanya asilimia 93. “Hivyo, niendelee kusisitiza menejimenti ya halmashauri kuongeza nguvu ya ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha kuwa asilimia saba iliyobaki inakusanywa kabla ya tarehe 30 Juni, 2025. Wataalamu wangu waliniambia hadi kufikia tarehe 31 Mei, jiji lilitakiwa kuwa na asilimia 90. Hivyo, jiji lilikuwa mbele kwa asilimia tatu. Tumebakiwa na muda mfupi kabla ya kukamilisha mwaka wa fedha, halmashauri iongeze wigo wa kusimamia miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa. Tunapoenda kukamilisha mwaka wa fedha tuhakikishe tunapeleka fedha za miradi ya maendeleo asilimia 70 na asilimia 10 ya mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu pamoja na fedha za lishe” alisisitiza Senyamule.

MWISHO

Comments

Popular Posts

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni nyenzo ya utendaji kazi serikalini – Dkt. Biteko

JIJI LA DODOMA KUPELEKA MIL 50 ZAHANATI YA KIKUYU

WENZA WA VIONGOZI WASHAURIWA KUANZISHA BUSTANI ZA NYUMBANI