Jiji la Dodoma lapata hati safi miaka mitatu mfululizo
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inajivunia kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wataalam na Baraza la Madiwani katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi ya fedha. Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA. David Rubibira alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA. David Rubibira alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa miaka mitatu ofisini kwake. CPA. Rubibira alisema “kwa bahati nzuri kwa kipindi cha uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ikipata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo. Hati inaangalia maeneo yafuatayo. Ukaguzi wa hesabu zilizowasilishwa na ukaguzi wa vitabu vilivyofanya malipo, nyaraka, viambata vyote na mchakato wa ukusanyaji mapato kama ulizingatia sheria, kanuni na taratibu. Hivyo, h...