Alhaj Shekimweri ahamasisha umuhimu wa mazoezi kwa wachezaji Dodoma Jiji FC
Na. Coletha Charles, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ameitembelea Timu ya Dodoma Jiji FC, inayondelea na mazoezi ya maandalizi ya msimu wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa lengo la kuwahamasisha wachezaji na viongozi wa timu kwa ajili ya kujiandaa vema. Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu kwenye uwanja John Merlin, Mkuu wa Wilaya alisisitiza umuhimu wa maandalizi mazuri kwa ajili ya msimu wa pili wa ligi kuu na kuwataka wachezaji kufanya mazoezi ili kuhakikisha wanapata mafanikio. Alisema kuwa, wanatakiwa kuweka mikakati yenye uhalisia kwa sababu wanaenda kwenye kipindi kibaya ambapo kusipokuwa na utulivu na maelewano wataishia kulaumiana na kushutumiana. “ Tunaenda ‘second round’ ya ligi yetu hatuko sehemu nzuri sana, hatuko sehemu mbaya sana katika mechi 16 nafikiri tuna ‘point’ 19 wastani wa ‘point’ moja kwa kila mechi. Kwahiyo, kuna haja ya kuwa familia moja kama alivyoongea mwalimu kwa kuelewa nini kipo mbele yetu. Tuna mechi 14 tu za kuju...