TAKUKURU YAIBUKA NA PROGRAM YA USHIRIKI WANANCHI KUKABILI VITENDO VYA RUSHWA
Na Tabitha Joshua, CHANG’OMBE Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imeanzisha programu iitwayo TAKUKURU Rafiki inayolenga kuongeza ushiriki wa wananchi katika kukabili vitendo vya rushwa kwa jamii. Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Michael Sanga Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Michael Sanga katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Chang’ombe iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Sanga alisema “TAKUKURU Rafiki ipo kwa lengo la kufikia wananchi kwa karibu na kutatua kero zao wenyewe ambazo zinapatikana katika idara zote, zinazopatikana katika kata hii. Vikao vyote vinavyohusu TAKUKURU Rafiki vinafanywa katika ngazi ya kata Mwenyekiti wake ni diwani wa kata na katibu wake anakuwa ni Afisa Mtendaji wa Kata”. Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe, Tunu Dachi aliishukuru Ofisi ya TAKUKURU kwa kuanzisha proramu hii kwasababu imeweza kuondoa kero za wananchi katika kata...