Na. Sofia Remmi, Dodoma RS Watanzania wametakiwa kuendelea kuitunza Tunu ya amani wakati nchi ikielekea kwenye zoezi la Kitaifa la uchaguzi mkuu huku wanasiasa wakitakiwa kufanya kampeni za kistaarabu ambazo hazichochei hasira na vurugu zisizo na tija. Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Taifa, Askofu Dkt. Venance Chande, aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kutoa taarifa ya kongamano lililoandaliwa na Idara ya Elimu ya Mahakama ya Kadhi na Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Askofu huyo alisema kuwa amani ndio msingi wa maendeleo ya Taifa lolote Duniani. “Sisi watanzania hatujazoea kugombana, tumezoea kuishi pamoja kwa umoja na upendo, hatujazoea kubaguana kwa misingi ya makabila au dini zetu, hayo ndiyo maisha tuliyoyazoea kuishi” alisema Dkt. Chande. Aidha, amewataka Wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu. “Wanasiasa, huu ni mwaka wa uchaguzi, kampeni zifanyike kistaarabu zisiwe za kuchochea hasira, washawishi kwa Ser...