Waganga Wakuu wamemtunukia Rais Tuzo, Dkt. Mpango awapongeza, atoa maelekezo mahususi
Na. John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo. Tuzo hiyo aliitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamo wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma. Mbali na tuzo hiyo pia Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama. Dkt. Mpango amewapongeza Waganga Wakuu nchini kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia wananchi huku akiwataka waendelee kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao. Alisisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana hali halisi ya uchumi. “Nawaelekeza Mawaziri ...