Maekelezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 yatolewa Jiji la Dodoma
Na. Asteris Frank, DODOMA Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko ametoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 kwa umma. Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa umma Akizungumza mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake leo tarehe 26 Septemba, 2024 kuhusu maekelezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 alisema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi amepewa mamlaka ya kutoa maelekezo kuhusu uchaguzi. “Maelekezo haya yanatolewa siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi, kwa lengo la kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa na kwamba wapiga kura Pamoja na wagombea wanapata taarifa zote zinazohitajika kwa wakati. Maelekezo haya yanafafanua hatua zitakazo ongoza mchakato wa uchaguzi, kuanzia uandikishaji wa wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea, uteuzi wa wagombea na tarehe ya siku ya uchaguzi. Maelekezo haya yanalenga kuto...