MABARAZA YA ARDHI YANAMCHANGO KATIKA KUSULUHISHA MIGOGORO YA ARDHI
Na. Eleuteri Mangi, WANMM Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Mabaraza ya Ardhi na Nyumba imeshiriki uzinduzi wa Wiki ya Sheria jijini Dodoma yakiongozwa na Mhe. Dkt. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika Januari 27, 2024 katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma ukitanguliwa na matembezi ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria ambao umehusisha viongozi mbalimbali wa mahama, watumishi wa umma na wananchi kutoka jiji la Dodoma. Akizungumzia ushiriki wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Dodoma Bw. Jackson Kanyerinyeri amesema kuwa moja ya jukumu lao ni kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hilo katika masuala ya ardhi, migogoro ya ardhi namna inavyotatuliwa katika mabaraza hayo hadi kutolewa hukumu. Bw. Kanyerinyeri ameongeza kuwa wamepata wasaa mujarabu wa kuwaeleza wananchi juu ya mabadiliko ya Sheria Na 3 ya 2021 ambayo imeondoa mamlaka ya mabaraza ya Kata kusikiliza ...