KAMPENI YA KILL CHALLENGE 2023 KUCHAGIZA JITIHADA ZA KUZIFIKIA SIFURI TATU DHIDI YA VVU NA UKIMWI

Na. Mwandishi Wetu Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amepongeza kampeni maalum ya kuchangia fedha katika utekelezaji wa afua za masuala ya UKIMWI nchini ya Kilimanjaro HIV & AIDS Challenge 2023 kwa kuzingatia mchango wake katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza wapanda Mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli kuzunguka mlima huo leo Julai 14, 2023 katika lango la Machame Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Kilimanjaro HIV & AIDS Challenge 2023 inayolenga kuchagia fedha kwa ajili ya masuala ya Afua za UKIMWI nchini.Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga Ametoa pongezi hizo mapema Julai 14, 2023 wakati wa hafla ya kuwaaga wapanda Mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli kuzunguka mlima huo katika lango la Machame Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kampeni hiyo kwa mw...