Mikakati ya Usalama Barabarani inalenga kudhibiti ajali
Na. Flora Nadoo, DODOMA Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo ameitaja mikakati ya usalama barabarani kuwa inalenga kudhibiti madereva walevi, wazembe na wanaoendesha kasi Pamoja na mambo mengine. Alizungumza hayo tarehe 26 Agosti, 2024 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani na Miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Sillo aliwataka madereva na wananchi wawe waangalifu na vyombo vya moto pamoja na sheria za barabarani ili kuepuka ajali za barabarani zisizo za lazima. “Mkakati wa Usalama Barabarani unalenga maeneo yafuatayo uthibiti wa madereva walevi na wanaoendesha kwa uzembe, uthibiti wa mwendokasi kwa madereva, kuwashirikisha wamiliki wa vyombo vya moto katika dhana ya uwajibikaji. Hii ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na madereva wenza kwa mabasi ya masafa marefu. Vilevile, kuthibiti uendeshaji wa magari bila sifa au kutokuwa na leseni...