Posts

Showing posts from September 15, 2023

MAKARANI UCHAGUZI MDOGO KATA YA NALA WAHIMIZWA UADILIFU

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MAKARANI wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Nala, Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu ili kufanikisha uchaguzi huo. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo alipokuwa akifungua mafunzo kwa makarani wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Nala yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kayombo ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “ninyi makarani tumewaamini, tumewapa ridhaa muende mkafanye kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa kabisa. Wakati tunawachagua tuliangalia sifa zenu, mliomba wengi. Mheshimiwa Jaji waliomba watu 1,500 lakini kupata hawa 12 ni mchakato ambao tumeufanya usiku na mchana mpaka kupata hawa 12 na wa akiba wawili. Siyo kwamba wale wengine hawana sifa hapana. Sifa moja wapo lazima awe raia wa Taznania, awe ...