Vikundi vya Kata ya Kizota vyapatiwa elimu ya mikopo ya 10%
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA Vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika Kata ya Kizota vimepatiwa elimu kuhusu taratibu za kuomba mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa robo ya pili ya mwaka, inayotarajiwa kutolewa katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2026. Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Lechasa, Kata ya Kizota, ikiwa na lengo la kuviandaa vikundi hivyo kuelewa taratibu na masharti ya mikopo hiyo ili viweze kunufaika na fursa zinazotolewa na halmashauri. Akizungumza katika semina hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Kizota, Ilumva Hoka amevihimiza vikundi kuendelea kujiandaa na kujisajili kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa ili viweze kutumia fursa hiyo kukuza shughuli zao za kiuchumi. Amesema kuwa katika kipindi hiki cha mwezi Oktoba, 2026 kiasi cha shilingi bilioni 7.5 kinatarajiwa kutolewa kwa ajili ya mikopo hiyo, huku katika Kata ya Kizota zaidi ya vikundi vitano vikitarajia kuwasilisha maombi ya mi...