Posts

Showing posts from July 31, 2023

JIJI LA DODOMA KUPELEKA MIL 50 ZAHANATI YA KIKUYU

Image
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KASKAZINI SERIKALI kupeleka shilingi milioni 50 kukamilisha jengo la wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kikuyu iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuwafikishia huduma za afya wananchi. Mbunge Anthony Mavunde Kauli hiyo ilitolewa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi wa mazingira na upandaji miti kuzunguka Zahanati ya Kikuyu. Mavunde alisema “Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma jengo unaloliona kushoto kwako ni jitihada zangu mimi na diwani wa hapa. Habari njema ni kwamba kabla ya Jumatano wiki ijayo tunaingiza shilingi milioni 50 ambazo zitakwenda kukamilisha jengo hilo. Na nategemea mwezi Oktoba mwaka huu kina mama wataanza kuhudumiwa katika wodi ya wazazi”. Akiongelea historia ya jengo hilo, alisema kuwa mwaka 2020 aliwaahidi wananchi wa kata hiyo kujengewa wodi ya wazazi. “Nilikuja hapa nikiwa na Diwani Mwansasu nikakut...

DC DODOMA APONGEZA ZAHANATI YA KIKUYU KUBORESHA MANDHARI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ameipongeza Zahanati ya Kikuyu kwa kuboresha mandhari na kuyafanya ya kuvutia na kupanda miti kwa lengo la kuwa na hewa safi. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shemimweri akiongea na mamia ya wananchi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini Pongezi hizo alizitoa alipoongoza zoaezi la usafi wa mazingira na kupanda miti katika zahanati hiyo iliyopo katika Kata ya Kikuyu Kaskazini jijini Dodoma. Shekimweri alisema “niungane na Mheshimiwa Mbunge kuwapongeza kwa dhati Zahanati ya Kikuyu ikiongozwa na Mganga Mfawidhi kwa wazo la kuboresha mandhari ya zahanati yao. Ni dhamira yetu tutafute ‘model’ ya uangalizi wa mazingira katika maeneo yetu ya kutolea huduma ya afya. Mbunge amening’ata sikio kuwa atabadilisha paa siyo kwa kupaka rangi bali yeye ataleta mabati mapya”. Aidha, alitoa rai kwa vituo vingine vya afya kuboresha mandhari yake. “Rai kwa vituo vingine vya afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuboresha mandhari. Mganga...

WANANCHI CHAMWINO WAJITOKEZA USAFI WA MAZINGIRA

Image
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO KATA ya Chamwino iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma yatekeleza zoezi la usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa wananchi kijitokeza kwa wingi na kufanya usafi katika maeneo ya jumuiya. Zoezi la usafi likiendelea Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa zoezi la usafi wa pamoja wa kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi lilifanyika katika mitaa minne ya kata hiyo. “Nikuhakikishie kuwa usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi umefanyika katika mitaa yote minne ya Kata ya Chamwino. Mtaa wa Nduka, Mailimbili, Sokoine na Mwaja” alisema Nkelege. Akiongelea maeneo yaliyofanyiwa usafi wa pamoja, aliyataja kuwa ni makorongo, kusafisha mitaro na maeneo ya biashara. “Mtaa wa Mwaja na Nduka iliungana na kufanya usafi wa pamoja katika korongo. Usafi huo ulihusisha kuondoa mifuko ya plastiki, kufyeka vichaka na nyasi zilizoota ndani ya korongo. Mtaa wa Mailimbili usafi wa pamoja ulifanyika katika mtaro wa barabara ya kwenda Arusha. Us...