Posts

Showing posts from August 6, 2024

Maendeleo ya Miradi Kata ya Makole

Na. Jackline Patrick, DODOMA Maendeleo ya kata ya makole yanatokana na serikali kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoboresha maisha ya wananchi. Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa kata ya Makole, Omary Haji alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya jiji la Dodoma kuhusu maendeleo ya kata ya makole. "Maendeleo ya Kata ya Makole yanatokana na miradi ya maendeleo ambayo imeanzishwa. Kata ina miradi mikubwa mingi kuna ujenzi wa madarasa kiwango cha ghorofa, uliogharimu takribani shilingi milioni 500. Tunamiradi tofauti tofauti ili kuweza kukamilisha miradi hiyo lazima kuwe na jitihada" alisema Haji. Vilevile, Kata ya Makole "inaujenzi katika eneo la D center na Ofisi ya wamachinga Jijini Dodoma. Katika maendeleo haya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo pia amechochea miradi kusonga mbele, haisuisui, miradi haina viporo na kukamilika kwa wakati" alisisitiza Haji. ...

Dodoma Jiji FC yaja kivingine

Image
Na. Fadiga James, DODOMA Timu ya Mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji ambayo imekuwa ikishiriki ligi kuu nchini imeweka mikakati mizito kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC premier league) unaotarajia kuanza hivi karibuni.   Mikakati hiyo ilitajwa na Diwani wa Kata ya Makole, Omary Haji alipokuwa akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhusiana na maandalizi ya Dodoma Jiji FC kuelekea kuanza kwa ligi kuu. Diwanni Haji alisema kuwa timu hiyo imejiwekea mikakati kwenye msimu mpya wa mashindano unaotarajia kuanza mwisho mwa mwezi Agosti, 2024 kuwa ni kushinda mechi zote. ‘Mimi kama mdau wa Dodoma Jiji FC kwanza najivunia na kujisikia fahari kuwa na timu inayoshiriki ligi kuu. Kwahiyo, cha kwanza wananchi wetu wa Dodoma watafurahia kuangalia mechi kwa timu zinazoshiriki ikiwemo Simba, Yanga na Azam na timu nyingine kwasababu lazima zije kucheza hapa. Sisi kama Dodoma Jiji FC tulikaa wakati tunavunja kambi na Mkurugenz...

Baraza la Madiwani Dodoma lampongeza Rais fedha za miradi

Image
Na. John Masanja, KATA YA VIWANDANI   Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lampongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuhakikisha serikali inapeleka fedha za kutosha katika maendeleo na kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali nchini hususani ndani ya Jiji la Dodoma.   Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata, uliofanyinya katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.   “Hakuna ubishi wowote kuhusu jinsi serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyopoleka pesa kwa ajili ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi, hili halina ubishi” alisema Prof. Mwamfupe.   Aidha, Pro. Mwamfupe aliwata wajumbe wa mkutano huo kuendelea kutoa u...

Madiwani Jiji la Dodoma washauriwa kushirikiana na wadau wa maendeleo

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo amewashauri madiwani kujenga uhusiano mzuri na wadau wa maendeleo waliopo katika kata ili wasaidie kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo akifafanua jambo Kayombo alitoa kauli hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Kayombo alisema “wadau wa maendeleo kwenye kata wapo wengi tuwatumie ili kuunga mkono utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata”. MWISHO

Wanafunzi wa ‘field’ wapelekwe kwenye kata

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amewataka wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenda kwenye kata kufanya kazi za jamii ili kupata uzoefu tofauti. Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe Kauli hiyo aliitoa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Prof. Mwamfupe alisema “idadi ya wanafunzi wa ‘field’ ni kubwa, waende kwenye kata kufanya kazi za jamii. Wapo waandishi wa habari hapa, habari hazipo kwa Mstahiki Meya na Mkurugenzi pekee, waende kwenye kata. Hii itawanufaisha wao kwa kupata uzoefu na kutakuwa na mafuriko ya habari zinazohusu kata na maendeleo ya wananchi”. Kwa upande wake Flora Nadoo alisema kuwa kauli ya Mshahiki Meya ni nzuri kwa sababu wanavyoenda kwenye kata wanajifunza vitu vingi na kujua changamoto zinazowakabili wananchi moja ...

Madiwani Jiji la Dodoma washauriwa kutafsiri miradi ya maendeleo kwa wananchi

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kutafsiri kwa vitendo maana ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kubadilisha maisha ya watu na kuyafanya kuwa bora kuliko jana. Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe akielezea miradi maana ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita. Kulia kwake ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ambae ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Joseph Fungo  Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe wakati akifungua mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili-Juni, 2024) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Prof. Mwamfupe ambae pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “hakuna ubishi wowote jinsi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu H...