Na. Leah Mabalwe, NALA Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Jiji la Dodoma, uliopo katika Kata ya Nala umegharimu kiasi cha shilingi 1,000,000,000 umekamilika na umeanza kutumika ukiwanufaisha wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari, Diwani wa Kata ya Nala, Herman Masila alisema kuwa hospitali hiyo ni msaada mkubwa kwa wananchi. “Kipekee nitoe pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya katika kata yetu ya Nala. Serikali imetupendelea sana kwa kutujengea hospitali kubwa na ya kisasa zaidi kwaajili ya wananchi wa Kata ya Nala na kata jirani wanaweza kupata huduma katika hospitali hii. Ni kweli wananchi tayari wameshaanza kupata huduma katika hospitali yetu na tunanufaika nayo” alisema Masila. Nea, Marry Kaka mwananchi wa Kata ya Nala akaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa mradi wa Hospitali ya Jiji la Dodoma. “Tunaishukurun sana serikali chini ya Rais, Samia, kwa kutujengea Hospitali ya Jiji kwenye kata yetu. Hospit...