Serikali ya Dkt. Samia inawajali wafanyakazi wa Sekta ya Afya
Na. Dennis Gondwe, MAKOLE SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inawajali wafanyakazi wa sekta ya Afya na kuthamini huduma wanazotoa kwa wananchi katika kuelekea kipindi cha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akiongea na waandishi wa habari Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa Kituo cha Afya Makole katika kuelekea kilele cha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Alhaj Shekimweri alisema “tunaposherehekea Uhuru wa nchi yetu, hawa wanaohudumiwa ni watanzania wenzetu ambao wapo huru. Hivyo, tunawajibu wa kuwasaidia ili wajifungue wakiwa salama na wengine wanaopata huduma mbalimbali za Afya. Serikali ya awamu ya sita inawajali na milango yetu ipo wazi kuwasikiliza pale mtakapohitaji kusikilizwa. Najua Mganga Mkuu, Dkt. Andrew Method anafanya kazi vizuri na sisi tunamtegemea sana na anawaunganisha vizuri. Najua mpo salama kwenye mi...