Mwenyekiti UWT Taifa awataka wanawake kuchangamkia mikopo ya Jiji la Dodoma
Na. Faraja Mbise. DODOMA Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda amewataka wanawake wafanyabiashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuachana na mikopo ya Kausha damu na mwendokasi inayowanyanyasa na kuwadhalilisha wanawake kutokana na muda wa marejesho na kiwango cha riba kuwa kikubwa na hivyo kushindwa kujikwamua kiuchumi na kuwaongezea umasikini zaidi. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza katika Uzinduzi wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara Masoko yote katika Jiji la Dodoma (UWAWAMA), uliofanyika Cathedral Social Hall, tarehe 01 Novemba, 2024. Chatanda aliwataka wanawake wafanyabiashara kuachana na mikopo ya kausha damu na kujiunga na vikundi ili kupata mikopo ambayo inatolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. "Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluh Hassan imerejesha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na ...