DG TANESCO atembelea Banda la EWURA CCC, apongeza utendaji kazi
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange, amelipongeza Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC), kwa mchango wake katika kupokea, kusaidia na kufuatilia utatuzi wa malalamiko ya watumiaji wa huduma za nishati na maji, hatua inayosaidia huduma zinazodhibitiwa na EWURA ikiwemo huduma ya umeme kuboreshwa kwa maslahi ya wananchi. Twange ametoa pongezi hizo leo, Juni 19, 2026, baada ya kutembelea banda la EWURA CCC katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. Akizungumza katika banda hilo, Twange amesema kazi inayofanywa na EWURA CCC ya kupokea, kusaidia na kufuatilia utatuzi wa malalamiko ya huduma za umeme imekuwa chachu ya maboresho ya huduma hiyo, ikiwemo kupungua kwa baadhi ya changamoto zilizokuwa zikilalamikiwa mara kwa mara. “Tunatambua mchango mkubwa wa EWURA CCC katika kuwawakikisha wananchi na kufuatilia utatuzi wa changam...