Posts

Showing posts from April 30, 2024

RC Senyamule aagiza utengenezaji Viti uende sambamba na ujenzi wa madarasa Sekondari Mtumba

Na. Dennis Gondwe, MTUMBA MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameagiza ujenzi wa madarasa uende sambamba ya utengenezaji wa viti na meza kwa ajili ya wanafunzi ili vyote vikamilike pamoja na kuanza kutoa huduma. Kauli hiyo aliitoa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mtumba iliyopo Kata ya Mtumba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Baada ya kukagua hatua ya ujenzi wa miundombinu hiyo alihoji hatua ya utengenezaji wa viti na meza ambao ulikuwa haujaanza. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliagiza utaratibu wa kutengeneza viti na meza uanze ili uende sambamba ya ujenzi wa miundombinu hiyo na kukamilika pamoja ili isicheleweshe utoaji wa huduma. Akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2024/2025 Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtumba, Mwl. Stephen Moshi alisema kuwa ujenzi unaendelea vizuri. “Shule ilipokea shilingi 201,000,000 tarehe 6 Ja...

RC Dodoma afurahishwa ujenzi Sekondari Mtemi Chiloloma

Na. Dennis Gondwe, HOMBOLO MAKULU MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameagiza ujenzi wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma kusimamiwa vizuri ili ukamilike katika muda uliopangwa kwa ajili ya kutoa huduma. Agizo hilo alilitoa alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo iliyopo katika Kata ya Hombolo Makulu, jijini Dodoma. Awali akikagua ujenzi huo alieleza kufurahishwa kwake na hatua ya ujenzi wa shule hiyo. Aliwataka viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kusimamia vizuri mradi huo ili uweze kukamilika katika muda uliopangwa. Akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba nane vya madarasa na matundu 18 ya vyoo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma, Mwl. Livinus Tanganyika alisema shule yake ilipokea shilingi 216,000,000 kutoka serikali kuu. “Ujenzi ulianza tarehe 25 Novemba, 2023 mpaka sasa ujenzi wa madarasa umekamilika kwa asilimia 100, matundu ya vyoo 18 yapo hatua ya umaliziaji, kazi inayoendelea ni kuweka mar...