Posts

Showing posts from August 4, 2024

Rais, Dkt. Samia: SGR siyo ndoto tena

Image
Na. Janeth Gerald, KIKUYU KUSINI Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua treni ya mwendokasi (Standard Gauge Railway) na kuandika historia baada ya miaka 114 ya Tanzania kujenga reli ndefu na kusema kuwa mradi wa SGR siyo ndoto tena, bali ni uhalisia. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miundombinu na safari za treni kati ya Dar es salaam na Dodoma kupitia Morogoro alisema kuwa aliupokea mradi huo kutoka kwa watangulizi wake na kuufikisha hapo. Alisema kuwa katika miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita, wamekamilisha ujenzi wa vipande viwili vya Dar es salaam hadi Morogoro na Morogoro hadi Dodoma. "Kwa sasa kazi inaendelea katika vipande vya Makutupora hadi Tabora kilometa 368, Tabora hadi Isaka kilometa 341, na Isaka hadi Mwanza kilometa 341. Pia serikali inajenga Tabora hadi Kigoma, kipande chenye urefu wa kilometa 565, ambayo itajumuisha kuingia katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Nchi zilizoendelea hazikutaka kuona Tanzania ina...

Rais Samia asisitiza kuendelezwa kwa ubora wa reli ya SGR

Image
Na. Fadiga James, KIKUYU KUSINI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirika la Reli nchini (TRC) kuhakikisha ujenzi wa reli ya SGR unaendelea kufanyika kwa ubora wa hali ya juu. Agizo hilo alilitoa wakati wa uzinduzi wa stesheni ya SGR Dodoma iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini jijini Dodoma. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa TRC na menejimenti yake kusimamia ujenzi wa reli ya SGR kwa ubora wa hali ya juu. Reli ikijengwa vizuri itaweza kudumu kudumu na kunufaisha nchi kwa muda mrefu, aliongeza. "Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya TRC, hakikisheni vipande vya reli hii inayoendelea kujengwa ya SGR, vinakamilika kwa wakati na ubora uliokubariwa" alisema. Vilevile, aliiagiza TRC kuhakikisha huduma zinazotolewa ndani na nje ya treni zinakuwa za ubora ili kuvutia zaidi watalii wa ndani na nje ya nchi na kuhakikisha usalama wa abiria na mali zao ndani ya treni hiyo. MWISHO

RC aishukuru Serikali kupeleka Nanenane kitaifa Dodoma

Image
Na. Fadiga James, NANENANE Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameishukuru serikali kwa kuamua maonesho ya Nanenane kitaifa kufanyikia Dodoma na kusema ni fursa kwa wananchi wa mkoa huo kunufaika kiuchumi. Senyamule alitoa shukrani hizo wakati akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kwenye ufunguzi wa maonesho ya Nanenane kitaifa yaliyofanyika Kanda ya Kati uliofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha sherehe za Nanenane kufanyika jijini Dodoma na kusema kuwa ni mahali sahihi kwasababu wakulima na wafugani ni wengi na yatasaidia wananchi kukua kiuchumi. “Kipekee nishukuru sana kwa dhati kuwa mwaka huu 2024 maonesho ya Nanenane yanafanyika Kanda ya Kati kitaifa katika Mkoa wa Dodoma. Tunashukuru sana kwasababu ni historia ya muda mrefu kidogo, tulishaanza kusahau kuandaa hata haya maonesho ya kimataifa, lakini tutoe shukrani nyingi kwa mheshi...