Bodaboda ni kazi, epukeni uhalifu

Na. Dennis Gondwe, MNADANI VIJANA waendesha Pikipiki (bodaboda) katika Kata ya Mnadani wametakiwa kuichukulia kazi ya kuendesha pikipiki kama kazi nyingine na kujiepusha na kujiunga kwenye makundi ya uhalifu. Picha kutoka mtandaoni Kauli hiyo ilitolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Focus Ishika alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Mnadani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo. Mkaguzi Msaidizi Ishika ambae pia ni Polisi Kata ya Mnadani alisema kuwa vijana waendesha bodaboda wanakosa elimu ya umuhimu wa kazi wanayofanya. “Vijana wetu wa bodaboda wanakosa elimu juu ya umuhimu wa kuichukulia kazi ya bodaboda kama kazi nyingine. Wazazi wenye watoto wanaoendesha pikipiki toeni elimu kwa vijana wenu ajira ya udereva pikipiki waichukulie kama yule anayeamka asubuhi na kwenda benki au kwenda kufundisha (mwalimu) wanatakiwa kuifanya kazi hiyo kwa moyo na bidii. Kwa hiyo makosa tunayo sisi. Mwanao anatoka asubuhi na pikipiki hujui anapaki kituo gani, hujui rafiki zake n...