Viwanda 17 vya kurejesha Taka za Plastiki vyaanzishwa Wilaya ya Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WILAYA ya Dodoma imefanikiwa kuanzisha viwanda 17 vya kurejesha taka za plastiki na kugawa vifaa 12 vya kutenganisha na kuhifadhi taka kwa lengo la kuweka mazingira safi na salama kwa shughuli na maisha kuendelea. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Kizota jijini Dodoma. Alisema kuwa wilaya kwa kushirikiana na wadau wa mazingira ilifanikiwa kuanzisha viwanda 17 vya kurejeresha taka za plastiki, kugawa vifaa 12 vya kutenganisha na kuhifadhi taka na elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi, mashirika na taasisi katika kudumisha utamaduni wa usafi na uhifadhi wa mazingira. “ Mheshimiwa Rais, wilaya inakadiriwa kuzalisha wastani wa tani 458 za taka ngumu kwa siku, ambapo wastani wa tani 305 sawa na asilimia 66.5 hupelekwa kwenye Da...