Posts

Showing posts from September 19, 2024

Uzinduzi ujenzi jengo la mapumziko Hospitali ya Mkoa wa Dodoma

Image
Na. Asteria Boniface, DODOMA MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde amezindua ujenzi wa jengo la mapumziko la wananchi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kusema kuwa ujenzi huo ni sadaka yake kwa wananchi. Alisema kuwa nje ya jengo hilo kuna eneo ambalo wanakaa wananchi ambao asilimia kubwa hawaishi katika Jiji la Dodoma na wanatumia sehemu ile kama sehemu ya kupumzikia kwaajili ya kusubiri muda wa kuwaona wagonjwa wao. Aliongeza kuwa wapo baadhi ambao hawana sehemu ya kulala na hawana makazi Dodoma na hawawezi kurudi walipitoka kwasababu ni mbali. Mbunge huyo alisema kuwa wakati mwingine wakina mama, baba na watoto wanachanganyikana na kulala sehemu moja. Alisema kuwa kulingana na maadili ya kitanzania sio vema sana kuchanganyika watu wa jinsi tofauti sehemu moja na hasa ambao kwa namna moja au nyingine hawana uhusiano wowote. “Mimi kama Mbunge, jambo hili lilinigusa sana nikasema moja ya sadaka, Mungu akinijalia na nitapenda niiache kama alama ni kiwahifadhi na k...