Watumishi wa Elimu watakiwa kuongeza tija kazini
Na. Mwandishi wetu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amewapongeza watumishi wa wizara hiyo kwa kazi kubwa na mafanikio waliyoyapata katika mwaka wa fedha uliopita, huku akiwataka kuendelea kuyasema kwa ujasiri mafanikio hayo yaliyoiwezesha sekta ya elimu kung’aa kitaifa na kimataifa. Prof. Nombo alisema kuwa mafanikio hayo yametokana na uongozi imara wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, na Naibu Waziri, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, pamoja na ushirikiano wa Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na watumishi wote. Prof. Nombo alisema hayo jijini Dodoma wakati alipoongoza kikao cha tafakuri cha uongozi na watumishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kilicholenga kutathmini utekelezaji wa majukumu yaliyokabidhiwa kwa wizara. Aliwashukuru watumishi kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yao na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano katika kufikia malengo ya wizara. Aidha, Prof. Nombo alisema kuwa mabadiliko makubw...