Posts

Showing posts from September 14, 2026

Ufaulu Elimu Sekondari wapanda Jiji la Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Ufaulu wa mitihani ya taifa kwa wanafunzi wa sekondari Jiji la Dodoma umeimarika kwa Mwaka 2025/2026, ambapo Division I, II na III zikiongezeka.   Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Vincent Odero wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 katika Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.   Alisema kuwa mwelekeo huo unaashiria maendeleo chanya katika sekta ya elimu ya sekondari, yakichangiwa na usimamizi mzuri wa elimu pamoja na juhudi kubwa za walimu katika kuboresha ufundishaji na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.   “Wanafunzi waliofanya mtihani waliongezeka kutoka 6,526 Mwaka 2024/2025 hadi 7,104 Mwaka 2025/2026, huku ufaulu wa ‘Division’ I, II na III ukiongezeka na ‘Division’ 0 na IV ukipungua. Hii inaashiria mwelekeo chanya unaoendelea,” alisema Odero.   Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Viwandani, Swal...

Jiji la Dodoma laimarisha huduma za afya, vituo vyafikia 163

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimeendelea kuimarishwa, huku vituo vikifikia 163 na watumishi wa afya wakiongezeka hadi 950 mwaka 2025/2026, kutoka 885 mwaka 2024/2025, hatua inayoongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi.   Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Vincent Odero wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 katika mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani, ambapo madiwani walipokea taarifa hiyo.   Alisema kuwa jiji limeendelea kuimarisha huduma za afya kupitia vituo vya serikali, mashirika ya dini, umma na binafsi, huku idadi ya watumishi ikiongezeka kutoka 885 hadi 950 kati ya mwaka 2024/2025 na 2025/2026.   “Jiji la Dodoma lina jumla ya vituo vya kutoa huduma za afya 163, hospitali zikiwa tisa, kati ya hizo hospitali tano ni za serikali, mbili ni za watu binafsi na mbili ni za mashirika ya dini. Vituo vya afya vipo 15, kati ya hivyo...

CCTV Camera zaimarisha usalama Jiji la Dodoma

Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Ufungaji wa kamera za CCTV katika maeneo mbalimbali umeendelea kuimarisha usalama, utii wa sheria za barabarani na ulinzi katika Jiji la Dodoma, huku madiwani wakipokea taarifa ya utendaji kazi wa TEHAMA.   Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Vincent Oderо wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 katika mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.   Alisema kuwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, maeneo 35 yalipangwa kufungwa kamera za CCTV, ambapo manne yalifungwa na maeneo 31 yakabaki kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, maeneo 31 yalipangwa kufungwa CCTV, ambapo 26 yamekamilika na maeneo matano bado hayajafungwa.   “Katika utekelezaji wa mifumo ya TEHAMA, kwa mwaka wa fedha 2024/2025, taasisi 287 kati ya 333 zilizopangwa zilifungiwa mifumo. Kwa mwaka wa fedha 2025/2026, taasisi 179 kati ya 227 zilizopangwa zimefungiwa m...

Madiwani Dodoma wapongeza ukusanyaji mapato na utekelezaji Bajeti ya 2025/2026

Image
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA   Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limepokea taarifa ya utendaji kazi wa halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2025/2026, huku wajumbe wakipongeza juhudi za menejimenti katika ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa bajeti.   Akiwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero alisema kuwa juhudi za ukusanyaji wa mapato zimeiwezesha halmashauri kutekeleza mipango na bajeti wake kwa ufanisi.   Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Aisha Msantu alisema kuwa menejimenti ya halmashauri imefanya kazi kubwa katika kukusanya mapato na kuhakikisha yanatumika kutekeleza bajeti.   “Nawapongeza kwa kazi kubwa ya kukusanya mapato na kuvuka lengo pia mmehakikisha yanatumika ipasavyo kutekeleza bajeti ya halmashauri” alisema Msantu.   Nae Diwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa ameipongeza menejimenti kwa utekelezaji wa bajeti na kusisitiza umuhimu wa kusimamia vyanzo vya mapato, ikiwemo Soko...

GCU Jiji la Dodoma yapongezwa umahiri katika kuhabarisha Umma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limekipongeza Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wananchi wanapata taarifa na habari kuhusu shughuli na utekelezaji wa majukumu ya halmashauri kwa wakati. Pongezi hizo zilitolewa na Diwani wa Kata ya Mnadani, Mugendi Kerenge wakati akichangia kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea na kuajdili taarifa ya utekelezaji wa kazi za halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.   Kerenge aliwapongeza wataalam wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa namna walivyokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na halmashauri.   “Nawapongeza wataalam wetu wa habari kwa namna wanavyofanya kazi nzuri ya kuhabarisha umma kwa wakati. Wananchi wamekuwa wakipata habari mbalimbali kutoka katika maeneo yao. Mfano, mimi habari za kata yangu zimeku...

Kliniki ya Kata ya Kikuyu Kaskazini kuwasogezea huduma wananchi mlangoni

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Wananchi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini Jijini Dodoma wanatarajiwa kunufaika na huduma mbalimbali za serikali kupitia Kliniki ya Kata itakayoanzishwa wiki hii ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwawezesha kupata huduma mbalimbali kwa urahisi. Hayo aliyazungumza Diwani wa Kata ya Kikuyu Kaskazini, Herry Beji nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa Kliniki hiyo itafanyika kwa muda wa wiki moja katika Shule ya Msingi Kikuyu, ambapo idara na taasisi mbalimbali zitashiriki katika kutoa huduma kwa wananchi, miongoni mwa huduma zitakazopatikana ni huduma za ardhi. “Lengo letu ni kusogeza huduma karibu na wananchi ili wasipate usumbufu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kutafuta huduma, ambapo wataalamu kutoka seksheni ya Ardhi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dodoma watakuwepo kusikiliza na kushughulikia changamoto mbalimbali za wananchi zinazohusu masuala ya Ardhi ...

Jiji la Dodoma lapongezwa kukusanya zaidi ya 100% mapato ya ndani Mwaka wa Fedha 2025/2026

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma yapongezwa kwa namna inavyosimamia na kukusanya mapato, hatua inayochangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji hilo kufuatia ukusanyaji wa zaidi ya asilimia 100 kwa bajeti ya mwaka 2025/2026. Pongezi hizo zilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum, Aisha Msantu mara baada ya kusomwa kwa taarifa ya tathmini ya mapato kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo. Alisema kuwa juhudi zinazoendelea kufanywa na halmashauri katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato zinapaswa kupongezwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia vyanzo vya mapato kwa ufanisi ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti na mipango ya maendeleo ya jiji. “Nipende kuwapongeza halmashauri kwa namna ambavyo wanaendelea kukusanya na kusimamia mapato. Lakini pia katika utekelezaji wa bajeti ya jiji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, tunaona juhu...

Ufaulu elimu ya msingi wapanda Jiji la Dodoma hadi 94.3%

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi Jiji la Dodoma umeongezeka katika mitihani ya PSLE na SFNA, ukifikia asilimia 93.32 na 94.3 kwa Mwaka 2025, kutoka asilimia 89.15 na 88.9 Mwaka 2021.   Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, kwenye mkutano wa Mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.    Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero alisema kuwa ongezeko hilo ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ya msingi, likionesha jitihada za halmashauri kuboresha elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.   “Ufaulu wa wanafunzi kwa miaka mitano kwa Darasa la Saba (PSLE) umeongezeka kutoka asilimia 89.15 kwa Mwaka 2021 hadi asilimia 93.32 Mwaka 2025. Aidha, ufaulu wa Darasa la Nne (SFNA) kwa miaka mitano umeongezeka kutoka asilimia 88.90 hadi asilimia 94.30, sawa na ongezeko la asilimia 5.4,” alisema Odero.   ...