Posts

Showing posts from August 8, 2024

CCM yampongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan utekelezaji Ilani

Na. Dennis Gondwe, DODOMA CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, John Mongela alipotoa salamu za CCM katika kilele cha maonesho ya Nanenane kitaifa, Nzuguni Dodoma. Mongela alisema “Ilani ya CCM ina kurasa 308, kurasa 33-56 zinaelezea sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Leo mimi ni shahidi kwamba utekelezaji wa Ilani unafanywa kwa kiwango cha juu sana, tumpongeze Rais na serikali yake. Chini ya uongozi wako ni kazi kubwa inatambulika kwenye sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Aidha, aliahidi CCM kuendelea kufanya kazi karibu na serikali ili wananchi wapate maendeleo zaidi. Akitoa salamu kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle alisema kuwa washirika wa maendeleo wanaunga mkono juhudi za Tanzania katika kukuza sekta za Kilimo,...

Jiji la Dodoma kidedea maonesho ya Nanenane 2024

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kinara wa tuzo na zawadi mbalimbali kwenye maonesho ya kimataifa ya Nanenane kutokana na kufanya vizuri katika maeneo mengi na kuwa kivutuo kwa wageni waliotembelea maonesho hayo. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufungua wa Trekta mkulima Dafalah S. Wadaa, Mkulima bora wa Kanda Kitaifa aliyezawadiwa Trekta na Bodi ya Pamba  Katika tuzo na zawadi zilizotangazwa mbele ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibuka mshindi katika vipengele sita vya mashindano ya Nanenane. Katika kipingele cha zawadi za wakulima bora kitaifa Kanda ya Kati iliyotolewa na Bodi ya Pamba, Dafalas Wadaa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma alizawadiwa zawadi ya Trekta. Kipengele cha wafugaji bora, mshindi wa kwanza aliibuka John Nassar kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuzawadiwa mitamba miwili yenye thamani ya shilingi 9,000,000, mashine ya kukamua yenye thamani ya shilingi 2,300,000 na fedha...

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha Matrekta jijini Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo kwa lengo la kusogeza matumizi ya matrekta karibu na wakulima nchini na kuwapunguzia gharama. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta Jiwe hilo la msingi liliweka na Rais katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma. Akitoa maelezo ya awali, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema kuwa kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo ni ushirikiano wa kampuni ya Agricom na Mahindra kutoka nchini India. Alisema kuwa makubaliano baina ya wizara yake na Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini, Angelina Ngalula ni kuwa kampuni hizo kufikia mwezi Juni, 2025 kiwanda hicho kianze kutoa huduma. Aidha, kiwanda cha kuunganisha matrekta kinajengwa katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Dodoma eneo lenye ukubwa w...